1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zanzibar yakamata mali za wafanyabiashara wa mihadarati

11 Novemba 2024

Mamlaka inayohusika na udhibiti wa dawa za kulevya visiwani Zanzibar imezitaifisha mali za raia mmoja wa Kijerumani kwa tuhuma za kuhusika na dawa za kulevya.

Zanzibar
Kilimo cha bangi kipo Paje Mkoa wa Kusini Unguja ambacho ni cha raia wa Ujerumani. Picha: Drug Control and Enforcement Agency

Kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Kanali Burhani Zuberi Nassoro, raia wa Ujerumani kwa jina la Andreas Wolfgang Fretz alikamatwa mwaka jana baada ya kugundulika ameanzisha kilimo cha kisasa cha dawa za kulevya aina ya bangi mseto kusini mwa kisiwa cha Unguja.

Miongoni mwa mali zilizotaifishwa ni gari, nyumba na fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 500 za Tanzania.

Mbali na raia huyo wa Ujerumani, mamlaka kwenye visiwa hivyo vya Bahari ya Hindi vimetaifisha mali za washukiwa wengine wawili wenyeji.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW