1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ZANZIBAR: Zoezi la kuandikisha wapiga kura

2 Aprili 2005

Zoezi la kuwaandikisha wapiga kura katika daftari la kudumu limeanza hii leo katika mkoa wa magharibi wa kisiwa cha Unguja huko Zanzibar.Mkoa huo yalipo makao makuu ya serikali ya Zanzibar ambayo ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,ndio wenye majimbo mengi zaidi ya uchaguzi kisiwani,kuliko mikoa 4 mingine,ukiwa na jumla ya majimbo 19.Zoezi hilo ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanywa nchini Tanzania,mwezi wa Oktoba mwaka huu.Kwa upande mwingine,hii leo polisi kisiwani Unguja walimkamata kwa muda Makamu wa rais wa chama kikuu cha upinzani-"Civic United Front"-bwana Machano Khamis Ali kwa kile kilichotajwa ni kuwepo kwa silaha nyumbani kwake pamoja na kuwaficha zaidi ya watu 100.Machano aliekamatwa pamoja na walinzi wake 3,waliachiliwa baada ya polisi kuipekua nyumba yake na kutogundua cho chote.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW