1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Zardari asema Taliban ''imevuka mstari mwekundu''

14 Machi 2026

Rais wa Pakistan Asif Ali Zardari amelionya taifa jirani la Afghanistan kwamba "limevuka mstari mwekundu" kwa kufanya mashambulizi ya droni kwenye maeneo ya raia nchini Pakistan.

Asif Ali Zardari,
Rais wa Pakistan Asif Ali Zardari katika picha kabla ya mkutano mjini Ankara, Uturuki mnamo Aprili 14, 2011Picha: AP

Zardari amesema wakati utawala wa Afghanistan unajaribu kujadiliana na mataifa jirani washirika wake, umevuka mstari mwekundu kwa kujaribu kuwalenga raia.

Kauli ya Rais Zardari ni ya hivi punde zaidi katika mapigano ambayo yamekuwa mabaya zaidi kuwahi kutokea kati ya nchi hizo mbili jirani.

Mapigano hayo ya mpakani, ambayo yalizuka mwishoni mwa mwezi uliopita, hayajaonyesha dalili za kupungua licha ya juhudi za China na Uturuki za kusimamia makubaliano ya kusitisha mapigano.

Shirika la habari la China Xinhua limeripoti kuwa hapo jana, waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi, alihimiza kutatuliwa kwa amani kwa mzozo huo kati ya Afghanistan na Pakistan, na kuonya kuwa matumizi ya nguvu yanazidisha mvutano na kutishia utulivu wa kikanda.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW