Zelenskiy akosoa uamuzi wa kuilegezea Urusi vikwazo
13 Machi 2026
Matangazo
Serikali ya Marekani ilitangaza mapema leo kuyaruhusu mataifa duniani kununua mafuta ya Urusi ambayo yamewekewa vikwazo na nchi za magharibi tangu kuzuka kwa vita vya Ukraine.
Akizungumza na waandishi habari mjini Paris akiwa pamoja na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, Zelenskiy amesema uamuzi huo utaipatia Moscow zaidi ya dola bilioni 10 inazoweza kuzitumia kwa vita.
Mtazamo wa Zelenskiy umeungwa pia mkono na Rais Macron pamoja na viongozi wengine wa Ulaya ambao wamekosoa hatua hiyo ya Marekani iliyochochewa na kupanda kwa bei za mafuta kutokana na vita vya Mashariki ya Kati.