1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelenskiy akutana na Papa Francis

11 Oktoba 2024

Rais Volodymyr Zelensky na kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis Ijumaa, wamejadili kuhusu suala la kurudishwa nyumbani raia wa Ukraine wanaoshikiliwa mateka Urusi.

USA New York 2024 | Ukrainischer Präsident Selenskyj spricht vor UN-Generalversammlung
Picha: Brendan McDermid/REUTERS

Mkutano wa Zelensky Vatican City ni sehemu ya ziara yake ya kuzunguka miji mikuu ya nchi za Ulaya akilenga kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa washirika wake kabla ya majira ya baridi kali.

Leo alasiri amekutana na Kansela Olaf Scholz mjini Berlin ambako, kiongozi huyo wa Ujerumani ameahidi kuipa Kiev msaada wa ziada wa silaha wa dola bilioni 1.5.

"Huu ni ujumbe wa wazi kwa Putin. Mchezo wa kuburuza muda ni hatua ambayo haitofanikiwa. Hatuwezi kuacha kuisadia Ukraine,'' alisema Scholz.

Zelensky anatafuta msaada zaidi wa kijeshi na kifedha katika ziara yake ya saa 48  London, Paris, Rome na Berlin, katikati ya kiwingu cha khofu ya kusitishwa msaada huo, ikiwa Donald Trump atashinda uchaguzi wa rais nchini Marekani mwezi ujao wa Novemba.