1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelenskiy asema nchi yake yahitaji silaha za masafa marefu

7 Julai 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema nchi yake inahitaji silaha za masafa marefu kukabiliana majeshi ya Urusi yaliyoivamia nchi yake.

Tschechien Volodymyr Zelenskiy und Petr Pavel
Picha: Michal Krumphanzl/CTK/dpa/picture alliance

Zelenskiy ameyasema haya katika ziara yake huko Jamhuri ya Czech, wakati ambapo Umoja wa Ulaya umesema utatoa yuro milioni 500 kwa ajili ya kuongeza utengenezaji wa silaha kwa ajili ya Ukraine.

Wawakilishi wa Baraza na Bunge la Ulaya wamefikia makubaliano hayo usiku wa kuamkia leo, na utekelezaji wake unatarajiwa kuanza kabla mwisho wa mwezi huu.

Haya yanafanyika wakati ambapo Ukraine imesitisha juhudi za uokoaji katika mji wa magharibi wa Lviv ambapo kulingana na Zelenskiy, idadi ya waliofariki kutokana na shambulizi la Urusi katika jengo moja la makaazi imefikia watu 10 sasa.

Polisi ya Ukraine inasema watu 45 wakiwemo watoto wamejeruhiwa katika shambulizi hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW