1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Zelenskiy: Tumepunguza uwezo wa wanajeshi wa Urusi Donetsk

20 Septemba 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema leo kuwa vikosi vya nchi yake vimepunguza uwezo wa wanajeshi wa Urusi wa kufanya mashambulizi katika mkoa wa mashariki wa Donetsk.

Deutschland Ramstein | Wolodymyr Selenskyj
Picha: Heiko Becker/REUTERS

Akizungumza kwenye hotuba yake ya kila siku kupitia njia ya video, Zelenskiy ameeleza kuwa vikosi vya Ukraine vinafanya kila linalowezekana ili kuzuia makali na kulirudisha nyuma jeshi la Urusi.

Ameongeza kuwa hali katika uwanja wa vita bado ni ngumu hasa karibu na mjini ya Pokrovsk na Kurakhove.

Soma pia: Von der Leyen kufanya ziara mjini Kiev siku ya Ijumaa 

Kiongozi huyo amefahamisha kuwa oparesheni ya vikosi vya Ukraine katika mkoa wa Kursk kusini mwa Urusi iliyoanzishwa mwezi uliopita, imefanikiwa kubadilisha mkondo wa jeshi la Urusi upande wa mashariki mwa Ukraine.

Amesema pia hatua ya kuwakamata wanajeshi wa Urusi kumeipa Ukraine sauti linapokuja suala la kubadilishana wafungwa wa vita na Moscow.