Zelenskiy asifu juhudi za Saudi Arabia za kuwa mpatanishi
28 Februari 2024Taarifa kutoka ofisi ya Rais Volodymyr Zelenskiy imeeleza kuwa viongozi hao wawili wamejadili juu ya mpango wa amani wa kumaliza mzozo huo ambao umeingia mwaka wake wa tatu huku Zelenskiy akitoa shukrani kwa Mohammed bin Salman kwa jukumu lake la upatanishi.
Shirika la habari la serikali ya Saudi Arabia limeripoti kuwa, utawala huo wa kifalme umejitolea kimasomaso kuunga mkono juhudi zote za kimataifa zinazolenga kuutatua mzozo kati ya Urusi na Ukraine.
Soma pia: Urusi yaandaa mashambulizi mapya dhidi ya Ukraine
Mohammed bin Salman amechukua jukumu muhimu kama mpatanishi wa mzozo huo, licha ya Saudi Arabia kuwa na uhusiano wa karibu na Urusi na kuunga mkono sera zake za nishati kupitia kundi la mataifa yanayozalisha mafuta kwa wingi duniani OPEC+.