1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelenskiy awasili Ujerumani

14 Mei 2023

Kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa vita vya Urusi na Ukraine, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy leo hii amewasili nchini Ujerumani

Berlin Besuch Präsident Selenzkyj
Picha: Lisi Niesner/REUTERS

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy  leo hii amepokelewa mjini Berlin na Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier katika ziara yake ya kwanza nchini Ujerumani tangu uvamizi wa Urusi, pale alipoanza safari za kuyatembelea mataifa washirika ya Ulaya katika jitihada yake ya kutafuta uungwaji mkono.

Zelenskiy aliwasili katikati ya usiku huko mjini Berlin akitokea Roma, ambapo alikutana na Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni, na Mkuu wa Kanisa Katoliki duniania, Papa Francis, ambaye alisema mamlaka ya Vatican itasaidia katika juhudi za kuwarejesha makwao watoto Ukraine waliochukuliwa na Warusi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW