1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelenskiy: Mataifa ya magharibi mnapaswa kutusaidia zaidi

2 Novemba 2024

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy amewatolea mwito washirika wake wa magharibi wasitazame tu bali wachukue hatua ya kukabiliana na uwepo wa wanajeshi wa Korea Kaskazini nchini Urusi.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy amewatolea mwito washirika wake wa magharibi wasitazame tu bali wachukue hatua ya kukabiliana na uwepo wa wanajeshi wa Korea Kaskazini nchini Urusi
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy amewatolea mwito washirika wake wa magharibi wasitazame tu bali wachukue hatua ya kukabiliana na uwepo wa wanajeshi wa Korea Kaskazini nchini UrusiPicha: Johanna Geron/REUTERS

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy amewatolea mwito washirika wake wa magharibi wasitazame tu bali wachukue hatua ya kukabiliana na uwepo wa wanajeshi wa Korea Kaskazini nchini Urusi kabla ya wanajeshi hao kuanza kutumika kwenye vita dhidi ya nchi yake.

Zelensky amesema Korea Kaskazini imepata maendeleo katika uwezo wake wa kijeshi, utumiajiaji wa makombora na utengenezaji wa silaha na sasa wanajeshi wake wanapata mafunzo yatakayowawezesha kushiriki kwenye vita na Urusi.

Soma zaidi.Korea Kaskazini yasema inaiunga mkono Urusi hadi mwisho 

Rais wa Ukraine amesema nchi yake imebaini eneo waliopo wanajeshi wa Korea Kaskazini lakini hawawezi kuwashambulia kwa sababu washirika wake wa magharibi hawajatoa silaha za masafa marefu ambazo wangezitumia kuwashambulia wanajeshi hao.

Kati kati mwa wiki hii Marekani ilisema kuna wanajeshi 10,000 wa Korea Kaskazini nchini Urusi wakiwemo 8,000 katika eneo la Kursk. Hapo jana Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini Choe Son Hui alimuhakikishia mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov kuwa nchi yake itasimama na Urusi hadi pale itakaposhinda vita vyake dhidi ya Ukraine.