1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelenskiy: Ukraine ilizaliwa upya baada ya uvamizi wa Urusi

24 Agosti 2022

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amewaambia Waukraine katika hotuba ya kuadhimisha miaka 31 ya uhuru kuwa nchi yao ilizaliwa upya wakati Urusi ilipoivamia na kuwa haitasalimisha uhuru wake kwa ubabe wa Moscow.

Ukraine | Wolodymyr Selenskyj
Picha: kyodo/dpa/picture alliance

Zelenskiy amesema vita vitamalizika tu sio wakati mapigano yatasitishwa bali wakati Ukraine itakapoibuka mshindi.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 44 amesisitiza msimamo mgumu wa Ukraineambao unapinga aina yoyote ya makubaliano ambayo yatairuhusu Moscow kudhibiti maeneo iliyoyakamata tangu kuanza kwa vita miezi sita iliyopita, yakiwemo maeneo ya kusini na mashariki mwa Ukraine.

Ameapa kuwa Ukraine italikomboa eneo liliokamatwa katika mkoa wa viwanda wa Donbas mashariki mwa nchi hiyo pamoja na rasi ya Crimea ambayo Urusi iliikwapua mwaka wa 2014.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW