JangaUlaya
Zelenskiy: Urusi imerusha makombora ya Korea Kaskazini
11 Agosti 2026
Matangazo
Zelenskiy ameyatoa madai hayo bila kutoa ushahidi.
Madai haya ya Zelenskiy yanakuja baada ya kudai kuwa Urusi inapokea makombora na majeshi kutoka kwa mwandani wake Korea Kaskazini.
Watu wengine 19 walijeruhiwa katika mashambulizi hayo yaliyofanywa katika mji wa Zaporizhzhia.
Ving'ora vilisikika katika miji ya Zaporizhzhia na Kyiv ambako gavana Ivan Fedorov amesema Urusi imefyatua makombora na mabomu ya angani.
Alichapisha picha za majengo na magari yakiwa yanateketea.
Kwengineko Ukraine mamlaka za serikali za mitaa zimeripoti kuwa watu wengine 6 wameuwawa na wengine 16 kujeruhiwa usiku wa kuamkia leo katika maeneo ya Dnipropetrovsk na Donetsk.