1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky adai Korea Kaskazini yaandaliwa kwa vita

17 Oktoba 2024

Zelenskiy adai jeshi Korea Kaskazini laandaliwa kujiunga na Urusi vita vya Ukraine.

Volodymyr Zelensky, rais wa Ukraine
Volodymyr Zelensky, rais wa UkrainePicha: Remko de Waal /ANP/IMAGO

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema Alhamisi kuwa nchi yake ina taarifa za kijasusi kuwa wanajeshi 10,000 kutoka Korea Kaskazini wanaandaliwa kujiunga na majeshi ya Urusi wanaopigana dhidi ya nchi yake.

Zelensky ameonya kuwa nchi ya tatu ikiingilia vita hivyo basi vitageuka na kuwa "vita vya dunia."

Zelensky ameyasema haya kabla kukutana na viongozi wa Umoja wa Ulaya kisha baadae mawaziri wa ulinzi wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO kuwasilisha ''mpango wake wa ushindi'' utakaomaliza vita vya Ukraine na Urusi.

Zelensky hakutoa taarifa zaidi kuhusiana na madai hayo ambayo ameyatoa siku moja baada ya naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani Kurt Campbell kusema Marekani na marafiki zake wanashtushwa na hatua ya Korea Kaskazini kuiunga mkono kijeshi Urusi.