1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Zelensky ahofia mashambulizi ya Urusi ya msimu wa baridi

Sylvia Mwehozi
13 Novemba 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema nchi yake inapaswa kujiandaa kwa msimu wa baridi, akihofia kwamba Urusi itaanza kampeni yake ya kushambulia miundombinu ya umeme.

Rais Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky Picha: president.gov.ua

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema nchi yake inapaswa kujiandaa kwa msimu wa baridi, akihofia kwamba Urusi itaanza kampeni yake ya kushambulia miundombinu ya umeme.

Katika hotuba yake ya kila siku aliyoitoa jana Jumapili, Zelensky amedai kwamba kuna uwezekano mkubwa adui yake akaongeza idadi ya mashambulizi ya droni na makombora na kuilenga miundombinu muhimu ya umeme.

Soma kwa kina: Urusi yazidisha mashambulizi katika mji wa Ukraine wa Avdiivka

Zelensky ametoa tahadhari hiyo wakati Kyiv ikisema kwamba inaimarisha ulinzi wake haswa wa mifumo ya anga. Taifa hilo limepokea mifumo muhimu ya ulinzi wa anga kutoka nchi za Magharibi, ikiwa ni pamoja na mfumo wa Patriot wa Marekani.

Mwaka jana vikosi vya Urusi vilifanya mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya gridi ya umeme ya Ukraine, na kusababisha maelfu kukosa nishati hiyo muhimu katika kipindi cha msimu wa baridi kwa muda mrefu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW