1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Zelensky aiomba NATO kuimarisha ulinzi kwenye maeneo yake

30 Novemba 2024

Rais Volodymyr Zelensky amesema Ukraine huenda ikakubaliana na Urusi kusitisha mapigano ikiwa Jumuiya ya kujihami, NATO itatanua ulinzi wake nchini humo.

Rais Volodymyr Zelensky amesema NATO inatakiwa kuutanua ulinzi wake hadi kwenye baadhi ya maeneo nchini humo ambayo bado yanadhibitiwa na Ukraine.

Zelensky amesema hayo siku ya Ijumaa katika mahojiano na kituo cha utangazaji cha Sky News cha nchini Uingereza.

Amesema wanatakiwa kufanya hivyo mara moja, na kuongeza, watatumia njia za kidiplomasia kuyarejesha maeneo yao yanayokaliwa na Urusi.

Amesema, mpango huo haukuzingatiwa hapo kabla kwa kuwa hakuna aliyewapendekezea rasmi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW