Zelensky aishukuru Marekani kwa msaada wa kijeshi
8 Julai 2023Ni baada ya Marekani kuthibitisha kuwa, mabomu ya mtawanyiko yatakuwa sehemu ya msaada huo mpya kwa Ukraine. Zelensky aliyetoa shukrani hizo kupitia ukurasa wake wa Twitter, ameielezea ahadi hiyo kuwa ni msaada mkubwa wa kujilinda unaohitajika kutoka Marekani.
Makundi ya haki za binadamu yamelaani uamuzi wa Marekani kuipatia Ukraine silaha za mabomu mtawanyiko , ambayo yanaweza kukaa muda mrefu bila kulipuka na kuhatarisha maisha ya raia katika miaka mingi ijayo kama sehemu ya msaada huo. Katibu mkuu wa Umoja wa Matafia pia amehoji juu ya uamuzi wa Washington.
Soma pia: Nini kitatokea iwapo Ukraine itajiunga na NATO?
Akiutetea uamuzi wa Marekani wa kuipatia Ukraine silaha hizo, ambazo ni sehemu ya msaada wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 800, mshauri wa usalama wa Marekani Jake Sullivan amesema kuna hatari kubwa ya raia kudhurika kama majeshi ya Urusi na magari ya kivita yataingia Ukraine na kujitwalia maeneo mengi zaidi