Zelensky aishutumu Korea Kaskazini kuipa Urusi silaha
14 Oktoba 2024Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameishutumu Korea Kaskazini kwa kutuma wanajeshi wake kujiunga na jeshi la Urusi na kwa mara nyingine tena akaomba msaada zaidi ili kuzuia "vita kubwa zaidi".
"Tunaona muungano unaoongezeka kati ya Urusi na tawala kama vile Korea Kaskazini. Sio tena kuhamisha silaha tu. Kwa hakika ni kuhusu uhamisho wa watu kutoka Korea Kaskazini hadi kwa vikosi vya kijeshi vya wavamizi. Ni wazi, katika mazingira kama hayo, uhusiano wetu na washirika wetu wanahitaji kuendelezwa Mstari wa mbele unahitaji msaada zaidi," alisema Zelenskiy.
Soma pia: Ukraine, Urusi zaidi kudunguliana ndege zisizotumia rubani
Kauli ya Zelensky inajiriki siku chache baada ziara yake ya katika miji mikuu kadhaa ya Ulaya kushinikiza ombi lake la msaada zaidi wa kijeshi na kifedha katika vita dhidi ya vikosi vya Urusi.
Haya yanajiri huku Urusi ikidai kuteka kijiji kingine cha mashariki mwa Ukraine wakati ikiendelea kukaribia mji muhimu wa Pokrovsk, ambapo vikosi vyake vimekuwa vikisonga mbele kwa wiki kadhaa.
Urusi imekuwa ikijaribu kuuteka mji huo wa kuchimba madini ambao ulikuwa na watu wapatao 60,000 kabla ya Moscow kuanza mashambulizi yake.