MigogoroUkraine
Zelensky aitaka Magharibi kuendeleza vikwazo kwa Urusi
15 Machi 2026
Matangazo
Akizungumza Jumapili, Zelensky amesema katika wiki moja tu, jeshi la Urusi lilirusha droni 1,770 pamoja na makombora 86 dhidi ya Ukraine. Aliongeza kuwa kila kombora lina angalau vipuri 60 vya kigeni vilivyopatikana kwa kukwepa vikwazo.
Wakati huo huo, Zelensky ameonya kuhusu vita vya Iran, akisema dunia haiwezi kuendelea kuweka mifumo ya ulinzi wa anga barani Ulaya na pia Mashariki ya Kati kwa wakati mmoja. Amesisitiza umuhimu wa kuzuia Urusi kutengeneza makombora mapya.
Baadhi ya washirika wa Ukraine, ikiwemo Ujerumani, pia wamekosoa uamuzi wa Marekani kuruhusu kwa muda mauzo ya mafuta ya Urusi, wakisema shinikizo kwa Moscow linapaswa kuendelea hadi vita vikome.