1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky aitaka Ujerumani kuuvunja ukuta wa Urusi

17 Machi 2022

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameisihi Ujerumani kusaidia kuubomoa ''Ukuta'' mpya ambao Urusi inaujenga barani Ulaya.

Deutschland Bundestag | Rede Wolodymyr Selenskyj
Picha: Markus Schreiber/AP Photo/picture alliance

Wito huo ameutoa leo wakati akilihutubia kwa hisia Bunge la Ujerumani kwa njia ya vidio. Zelensky amewaambia wabunge kwamba huo sio ''Ukuta wa Berlin'', ni Ukuta katikati ya Ulaya baina ya uhuru na utumwa na ukuta huo unakuwa mkubwa kutokana na mashambulizi ya mabomu ya kila siku yanayodondoshwa Ukraine.

Zelensky amemtaka Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, kuuvunja Ukuta huo, akikumbushia ombi la Rais wa zamani wa Marekani Ronald Regan alilolitoa kwa Mikhail Gorbachev la kuvunjwa kwa Ukuta wa Berlin wakati wa Vita Baridi.

Pia ameitolea wito Ujerumani kuunga mkono juhudi za Ukraine kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Aidha, Zelensky ameikosoa Ujerumani kwa kuchelewa kuufuta mradi wenye utata wa bomba la gesi unaogharamiwa na Urusi na Ujerumani unaojulikana kama Nord Stream 2.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW