1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky alenga kufufua mazungumzo ya amani

18 Novemba 2025

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema leo kuwa atafanya ziara nchini Uturuki kesho Jumatano kwa lengo la kufufua mazungumzo ya amani pamoja na mchakato wa kubadilishana wafungwa wa vita kati ya nchi yake na Urusi.

Ukraine Kiev 2025 | Zelensky katika mkutano na waandishi wa habari
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Tetiana Dzhafarova/AFP

Katika ujumbe aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii, Zelensky amesema wanajiandaa kutia nguvu mpya katika mazungumzo hayo na kwamba pia wameandaa suluhisho wanalotaka kupendekeza kwa washirika wao.

Zelensky ameongeza kuwa wanafanya kazi kurejesha mchakato wa kubadilishana wafungwa wa vita na kuwarudisha wafungwa wao nyumbani.

Mabadilishano ya wafungwa na kurejeshwa nyumbani kwa miili ya wanajeshi waliofariki ndio matokeo ya pekee yanayoonekana ya mazungumzo kati ya wajumbe wa Urusi na Ukraine mjini Istanbul kati ya Mei na Julai.

Hakukuwa na majibu ya haraka kutoka kwa Urusi kuhusiana na taarifa ya Zelensky.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW