1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky amfuta kazi balozi wake nchini Uingereza

21 Julai 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amemfuta kazi balozi wao nchini Uingereza Vadym Prystaiko baada ya kukosoa jibu la rais kuelekea mvutano wa msaada wa kijeshi wa Uingereza nchini Ukraine.

Ukraine I Volodymyr Selenskyj
Picha: Sergei Supinsky/AFP

Prystaiko alikosoa jibu la kejeli la Zelensky kufuatia mapendekezo ya waziri wa ulinzi wa Uingereza Ben Wallace kwamba Ukraine inapaswa kuonyesha shukrani zaidi baada ya kupewa silaha na washirika wake.

Soma pia: Zelensky asifu ujasiri wa Ukraine siku 500 za vita

Zelensky amesaini amri ya kufukuzwa kwa balozi huyo iliyochapishwa katika tovuti ya raia, ingawa haikueleza sababu hasa ya kufukuzwa kwake.

Mvutano huo ulianza baada ya Wallace kusema katika mkutano wa kilele wa NATO huko Vilnius mwezi huu kwamba Uingereza sio kama kampuni ya usafirishaji bidhaa ya Amazon ya kupeleka silaha Ukraine na kupendekeza Kyiv inatakiwa kushukuru sana, matamshi yaliyojibiwa na Zelensky aliyesema hajui namna nyingine ya kushukuru.