1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky anasema anataka kumaliza vita kwa diplomasia

16 Novemba 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kuwa angetamani vita na Urusi vimalizike mwaka ujao kwa njia za kidiplomasia, hasa wakati nchi zote mbili zikijiandaa kwa Donald Trump kurejea Ikulu.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky atamani vita na Urusi vimalizike kwa njia za kidiplomasia.Picha: Remko de Waal /ANP/IMAGO

Matarajio ya Trump kurejea madarakani yameibua maswali kuhusu hatma ya mzozo huo, kutokana na Mrepublican huyo kukosoa waziwazi msaada wa kijeshi kwa Kyiv.

Zelensky alizungumzia umuhimu wa diplomasia huku akikataa masharti ya Rais wa Urusi Vladimir Putin ya kuitaka Kyiv kuachia maeneo yalitwaliwa na Urusi.

Soma pia: Zelensky aelezea kusikitishwa na mazungumzo ya Scholz, Putin

Wakati huo huo, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alifanya mazungumzo ya simu na Putin, licha ya pingamizi kutoka Ukraine, ambayo iliiona hatua hiyo kama jaribio la kumfurahisha Putin.

Soma pia: Tahadhari ya mashambulio ya anga yatolewa kote Ukraine

Wakati mzozo ukiendelea, Zelensky amesisitiza hasara kubwa zinazovikabili vikosi vya Urusi,  huku mataifa ya G7 yakirudia msimamo wake wa kuiunga mkono Ukraine, na kuilaumu Urusi kama kikwazo pekee cha amani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW