1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky apuuza taarifa za Urusi kuteka kijiji mkoani Sumy

Hawa Bihoga
10 Juni 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amepuuzilia mbali taarifa za Urusi kuhusu kukiteka kijiji katika mkoa wa kaskazini mashariki mwa Ukraine Sumy, akisema bendera ya Urusi iliyokuwa ikipepea eneo hilo imeharibiwa vibaya.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Nhac Nguyen/AFP/Getty Images

Kupitia mtandao wa Telegram Rais Zelensky ameandikwa kwamba hadi kufia asubuhi ya leo bendera ya Urusi iliokuwa ikipepea katika kijiji cha Ryzhivka iliharibiwa vibaya na kwamba vikosi vyake viliwaondoa wakaaji katika eneo hilo linalozozaniwa na pande zote.

Zelensky aliongeza kwamba ushindi unaodaiwa kutangazwa na Urusi katika kijiji hicho unatajwa kuwa ni propaganda.

Hapo jana kiongozi katika Jamhuri ya Chechnya yenye mamlaka ya ndani Ramzan Kadyrov alisema kwamba kitengo maalum cha jeshi la Urusi kiliteka kijiji cha mpakani cha Ryzhivka kilichopo kwenye mkoa wa Sumy na kusababisha hasara kubwa kwa vikosi vya Ukraine.

Hata hivyo waangalizi wa masuala ya kijeshi walitilia shaka tangazo la kiongozi huyo ambae ni mshirika wa karibu wa rais wa Urusi Vladmir Putin, ingawaje kwa wiki kadhaa sasa kumekuwa na uvumi kuhusu wanajeshi wa Urusi kuanzisha makabiliano katika mkoa wa Sumy.

Urusi na Ukraine zashambuliana

Katika hatua nyingine Wizara ya Ulinzi Urusi imetangaza vikosi vyake kuanzisha mashambulizi kadhaa katika maeneo mbalimbali kwenye uwanja wa vita na kusababisha uharibifu mkubwa wa vifaru kadhaa vya Ukraine, magari ya kivita na makombora yaliotengenezwa na Marekani.

Wanajeshi wa Ukraine wakiuhifadhi mwili baada ya Urusi kuvyatua makombora kadhaa eneo la Kharkiv.Picha: Andrii Marienko/AP/picture alliance

Zaidi ya hayo vikosi vya Urusi pia vilisema viliwalenga waendeshaji wa ndege zisizo na rubani za Ukraine na kuyashambulia maeneo yanayokaliwa na mamluki wa kigeni.

Ukraine imesema pia kikosi chake cha anga kilizua mashambulizi kadhaa ya Urusi na kuimarisha safu ya mbele kwenye uwanja wa vita huko Kharkiv.

Mshauri wa masuala ya usalama wa Rais wa Marekani Joe Biden, Jake Sullivan, amesema kwamba vikosi vya Urusi "vimekwama" katika kusonga mbele kwenye eneo la mpaka wa Kharkiv  baada ya Washington kuondoa vikwazo kwa Kyiv kutumia silaha zilizotolewa na Marekani kushambulia ndani ya Urusi.

"Kharkiv bado ipo kwenye kitisho, lakini vikosi vya Urusi havijasonga mbele kwenye uwanja wa vita katika siku za karibuni." Alisema Sullivan.

Aliongeza kuwa "Marekani itaendelea kuiunga mkono Ukraine kwenye uwanja wa vita na kuvirudisha nyuma vikosi vya Urusi."

Juhudi za kidiplomasia zashika kasi tena

Katika kile kinachotazamwa kama kutafuta amani ya kudumu nchini Ukraine mataifa yapatayo tisini yamethibitisha kuhudhuria mkutano wa kilele wa amani wa Ukraine ulioandaliwa na Uswisi utaofanyika mwishoni mwa juma, ingawaje Urusi imekataa kushiriki mkutano huo, hadi pale masharti yake yatakapozingatiwa na Ukraine.

Kutibu majeraha yaliosababishwa na vita Ukraine

02:59

This browser does not support the video element.

Rais wa Uswisi Viola Amherd amewaambia waandishi wa habari kwamba mkutano huo utaofanyika siku ya Jumamosi na Jumapili, utalenga kutafuta njia ya kufikiwa kwa amani ya kudumu badaa ya vikosi vya Urusi kuvamia Ukraine kwa miaka miwili sasa.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW