MigogoroUkraine
Zelensky: Wanajeshi wanazingatia sheria za kiutu vitani
15 Agosti 2024Matangazo
Rais Zelenskyy amesema suala hilo tayari lilijadiliwa kwenye mkutano na viongozi wa Ukraine lakini pia misaada wa kiutu imeandaliwa kwa ajili ya raia walioko kwenye eneo kubwa la Ukraine linalodhibitiwa na Urusi.
Rais huyo wa Ukraine amesema wawakilishi wa mashirika ya kimataifa wanaweza kuruhusiwa kuingia kwenye maeneo hayo ili kufanya tathmini.
Maafisa wa Ukraine wamesema, Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu, Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa yanayotoa misaada ya kiutu yanaruhusiwa kuingia kwenye eneo la Kursk linalokaliwa na Ukraine.