Zelensky: Mazungumzo ya amani ya Ukraine yatakuwa mazuri
14 Februari 2026
Matangazo
Zelensky amesema ana matumaini makubwa kwamba mazugnumzo hayo yanayosimamiwa na Marekani yatakuwa na uzito na yenye umuhimu mkubwa.
Hata hivyo rais wa Ukraine ameonyesha wasiwasi kwamba ni nchi yake tu ndio mara zote inatakiwa ikubali kupunjika ili kufikia muafaka.
Zelensky amesema jambo hilo halimfurahishi na amesisitiza kwamba Ukraine haitakubali kuachia maeneo yake ya mashariki.
Rais wa Ukraine ameyasema hayo katika hotuba yake kwenye Mkutano wa Usalama wa Munich.
Amesema Marekani ambayo inasimamia mazungumzo hayo ya pande tatu mara nyingi mada hiyo ya kufikia makubaliano hujadiliwa tu katika muktadha wa Ukraine na sio Urusi.