1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky asema hakuna uwezekano wa vita kusimama

11 Januari 2024

Rais wa Ukraine Volodomyr Zelensky amesema leo kwamba hakuna uwezekano wa kusitishwa kwa muda vita kati ya nchi yake na Urusi akionya hatua hiyo itaiwezesha Moscow kujiimarisha na kuwa na uwezo mkubwa zaidi.

Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymir ZelenskyPicha: AFP/Getty Images

Rais wa Ukraine Volodomyr Zelenksy amesema leo kwamba hakuna uwezekano wa kusitishwa kwa muda vita kati ya nchi yake na Urusi akionya hatua hiyo itaiwezesha Moscow kujiimarisha na kuwa na uwezo mkubwa zaidi.

Ameyatoa matamshi hayo akiwa ziarani nchini Estonia, kituo cha pili cha ziara yake kwenye mataifa matatu ya kanda ya Baltiki yenye dhamira ya kutafuta nyongeza ya msaada wa kijeshi kwa nchi yake.

Kwenye mkutano na mjini Tallin akiwa pamoja na rais Alar Karis wa Estonia, Zelenksy amesema:

"Tutoe mapumziko? Tufanye bahati nasibu? Tuipe Urusi miaka miwili au mitatu? Hilo litawapa uwezo wa kutusambaratisha baadaye, kwa kweli hatuwezi kuchukua uamuzi kama huo wa kubahatisha", alisema Zelensky.

Matamshi ya kiongozi ambaye anatarajiwa jioni kuelekea nchini Latvia yanaashiria kutowepo uwezekano wa kusimama kwa vita kati ya Ukraine na Urusi ambavyo mnamo Februari 24 mwaka huu vitatimiza mwaka wa pili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW