Zelensky asema upo uwezekano wa makubaliano juu ya Crimea
28 Agosti 2023Matangazo
Aliyasema hayo kwenye mahojiano ya siku Jumapili (Agosti 27) na kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari vya nchini humo mapema Jumatatu.
Zelensky alisema angelipendelea suluhu ya kisiasa kwa ajili ya Crimea kwa kuwa itahusisha wahanga wachache.
Soma zaidi: Putin ataka wapiganaji binafsi kula kiapo kwa taifa
Rais huyo wa Ukraine alisisitiza kwamba hakutaka kuvihamishia vita kwenye ardhi ya Urusi kwa kuwa lengo lao ni kuyakomboa maeneo ya Ukraine.
"Ikiwa tungelisonga mbele hadi kwenye maeneo ya Urusi, wangelihatarisha kukosa misaada kutoka Magharibi." Alisema Zelensky.