1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky asema Urusi imerusha droni 3,500 mwezi Septemba

16 Septemba 2025

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema tangu mwezi Septemba uanze, Urusi imeishambulia nchi yake kwa zaidi ya droni 3,500 na makombora 190.

Zelensky ataka ulinzi mkali wa angani kuzuia maelfu ya droni yanayorushwa na Urusi
Zelensky ataka ulinzi mkali wa angani kuzuia maelfu ya droni yanayorushwa na UrusiPicha: Julien Mattia/Le Pictorium/MAXPPP/picture alliance

Rais Volodymyr Zelensky ameandika hayo kwenye ukurasa wake wa X na kuongeza kuwa kumekuwa pia na visa vya uchokozi wa Urusi dhidi ya washirika wa Ukraine.

Zelensky ameendelea kuwatolea wito washirika wake kusaidia nchi yake katika kuimarisha ulinzi wa angani ili kuzuia mashambulizi ya Urusi.

Huku mzozo wa Urusi na Ukraine ukiendelea, vikosi vya Urusi vimefanya mashambulizi makali mapema Septemba 16 kusini mashariki mwa mji wa Zaporizhzhia nchini Ukraine.

Gavana wa jimbo hilo Ivan Fedorov amethibitisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi 13, wakiwemo watoto wawili kutokana na mashambulizi hayo.

Fedorov amesema ripoti za awali zimesema magorofa 10 na majengo 12 binafsi yaliharibiwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW