1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky: Urusi inawaua raia bila huruma huko Kherson

21 Februari 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameishambulia Urusi kwa matamshi makali leo akisema inawaua raia bila huruma kwenye jimbo la Kherson.

Ukraine Präsident Selenskyj
Picha: Ukraine Presidency/Zuma/picture alliance

Katika ujumbe kupitia mtandao wa Telegram, Zelensky amesema kwa mara nyingine makombora ya Urusi yameyalenga maeneo ya makaazi, maegesho ya magari na vituo vya usafiri wa umma na kuhujumu maisha ya watu huko Kherson.

Duru za kijeshi zimearifu mashambulizi hayo yalifanywa wakati rais Vladimir Putin alipokuwa akitoa hotuba mjini Moscow ambapo amekaririwa akisema nchi yake haiko vitani na umma wa Ukraine.

Ukraine ilirejesha udhibiti wa mkoa huo wa kusini Novemba iliyopita baada ya kukamatwa na Urusi katika wiki za kwanza za uvamizi wa Moscow nchini humo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW