1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Zelensky asema wanajeshi wake wanakabiliwa na wakati mgumu

27 Julai 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema leo kuwa wanajeshi wake wanakabiliwa na wakati mgumu katika uwanja wa mapambano kutokana na mashambulizi ya Urusi mashariki mwa nchi hiyo.

Ukraine | Krieg | PK Präsident  Wolodymyr Selenskyj in Kiew
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Sergei Supinsky/AFP/ Getty Images

Katika hotuba yake kwa taifa kwa njia ya video, Zelensky ameeleza kuwa hivi karibuni maeneo karibu na mji wa Pokrovsk katika mkoa wa Donetsk yamelengwa na vikosi vya Urusi.

Kiongozi huyo ametoa mwito wa kuimarisha ulinzi zaidi katika maeneo hayo.

Soma pia: China yajadili mipango ya amani na Ukraine 

Kauli ya Zelensky ameitoa baada ya idara ya ujasusi ya Ukraine kueleza mapema leo kuwa vikosi vya Urusi vimelekeza nguvu zaidi katika eneo la Donbass mashariki mwa nchi hiyo na lenye utajiri wa makaa ya mawe.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW