1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Zelensky asema watu wanne wameuawa na 92 wajeruhiwa

2 Januari 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema watu wanne wameuawa na wengine wapatao 92 wamejeruhiwa kutokana na mashambulio makubwa ya makombora yaliyofanywa na Urusi.

Ukraine, Kharkiv
Athari za mashambulizi ya Urusi katika mji wa Kharkiv, Ukraine.Picha: Sergey Bobok/AFP

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema watu wanne wameuawa na wengine wapatao 92 wamejeruhiwa kutokana na mashambulio makubwa ya makombora yaliyofanywa na Urusi.

Zelenskiy amesema Urusi ilitumia ndege za droni zipatazo 170 aina ya Shahed. Ameeleza kuwa Urusi pia imetumia aina mbalimbali ya makombora tangu tarehe 31 mwezi Desemba.

Rais huyo wa Ukraine amewashukuru washirika wake kwa kuimarisha ulinzi wa anga wa nchi yake unaookoa maisha ya mamia ya watu kila siku.

Amesema maisha ya watu hao yangelipotea bila ya mfumo wa ulinzi wa makombora ya Patriots na mifumo mingine ya ulinzi.

Jeshi la anga la Ukraine pia limesema Urusi ilitumia makombora ya mwendo wa kasi kubwa kuushambulia mji mkuu Kiev. Meya wa mji huo Vitali Klitschko ameeleza kuwa watu wapatao 16 walijeruhiwa katika mashambulio hayo na wamelezwa hospitali. Miundombinu ya kiraia kadhaa pamoja na bomba la gesi limeharibiwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW