1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Zelensky aonyesha utayari wa kubadilishana wafungwa na Urusi

13 Januari 2025

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema yuko tayari kuwarejesha nchini mwao wanajeshi wawili wa Korea Kaskazini waliotekwa, kwa mabadilishano ya kuachiliwa huru wafungwa wa kivita raia wa Ukraine walioko Urusi.

Brüssel | 2024 | Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: John Thys/AFP

Pendekezo la Zelensky amelitoa saa chache baada ya idara ya kitaifa ya ujasusi ya Korea Kusini kuthibitisha tangazo la siku iliyopita kwamba Ukraine imewakamata wanajeshi wawili wa Korea Kaskazini.

Mamlaka nchini Ukraine imesema wanajeshi hao wawili walijeruhiwa vibaya katika uwanja wa vita wakati wakipambana na wanajeshi wa Ukraine katika eneo la Kursk nchini Urusi.

Soma pia: Zelensky atoa wito kwa utengenezaji wa droni Ukraine 

Zelensky ameandika katika mtandao wa kijamii kwamba wanajeshi wa Korea Kaskazini ambao hawataki kurudi nyumbani na wanaoonyesha nia ya kuleta amani kwa kueleza ukweli kuhusu vita hivyo nchini mwao, watapewa kile alichokiita "fursa nyengine."

Alipoulizwa mwaka jana kuhusu ushiriki wa wanajeshi wa Korea Kaskazini, Rais wa Urusi Vladimir Putin hakukanusha wala kukiri kwamba nchi hiyo inatumia wanajeshi wa Korea Kaskazini katika vita vyake dhidi ya Ukraine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW