MigogoroUkraine
Zelensky ataka mbinyo dhidi ya Moscow baada ya mashambulizi
25 Machi 2026
Matangazo
Zelensky alisema Jumanne kwamba "kiwango cha shambulio hilo kinaonyesha wazi kwamba Urusi haina nia ya kukomesha vita." Mfululizo wa mashambulizi ya anga ya Urusi usiku kucha ulifuatiwa na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani wakati wa mchana, ikiwa ni pamoja na kituo cha kihistoria cha jiji la magharibi la Lviv. Jeshi la Ukraine lilisema Urusi ilirusha droni 550 mchana kweupe ikiwa ni kinyume na mbinu iliyozoeleka ya kushambulia nyakati za usiku.
Mji mkongwe wa Lviv ni Eneo la Turathi za Dunia za UNESCO na uliongezwa kwenye orodha ya maeneo yaliyo hatarini kutoweka mwaka wa 2023 kutokana na uvamizi wa Urusi, ambao umekuwa ukiendelea kwa zaidi ya miaka minne.