1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky ataka ulinzi katika usafirishaji nafaka za Ukraine

2 Novemba 2022

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ameurai ulimwengu kujiweka tayari kujibu jarabio lolote la Urusi la kuvuruga usafirishaji wa nafaka ya Ukraine.

Ukraine-Krieg Odessa | Warten auf erste Getreide-Exporte | Präsident Selenskyj
Picha: UKRAINIAN PRESIDENTIAL PRESS/REUTERS

Ameyasema haya siku kadhaa baada ya Moscow kutangaza kujitoa kutoka kwenye mkataba ulioruhusu kusafirishwa tena kwa bidhaa za Ukraine.

Katika ujumbe wa video aloutoa usiku wa kuamkia Jumatano, Zelensky amesema hadi sasa meli zinazobeba shehena ya nafaka na bidhaa nyingine bado zinaingia na kutoka katika bandari za Ukraine lakini usalama wa muda mrefu wa njia ya bahari zinakopita unahitajika.

Amesema Urusi ni lazima ifahahamishwe kwamba dunia haitokaa kimya iwapo itathubutu kuvuruga usafirishaji wa nafaka na bidhaa za Ukraine zinazotegemewa na mamia kwa mamilioni ya watu duniani.

Urusi ilitangaza kusitisha ushiriki wake kwenye mkataba wa kusafirisha nafaka za Ukraine mwishoni mwa juma lililopita baada ya kuituhumu Kyiv kuzishambulia meli zake zinazopiga doria kwenye Bahari Nyeusi.