1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky ataka viongozi wa dunia kuchukua hatua haraka

13 Aprili 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametaka viongozi ulimwenguni kuchukua hatua baada ya video iliosambaa mtandaoni, inayodaiwa kumuonesha mfungwa wa vita wa Ukraine akichinjwa na mwanajeshi wa Urusi.

Ukraine Präsident Wolodymyr Selenskyj
Picha: Omar Marques/Getty Images

Rais Zelensky ameitaja video hiyo ambayo imezusha hasira miongoni mwa washirika wa Kyiv na Umoja wa Mataifa, si bahati mbaya kwa Urusi na kutaka viongozi wa dunia kuchukua hatua za haraka na kusisitiza kwamba lazima kuwe na hukumu kwa kile alichokiita "wauwaji" kwa taifa la waovu.

Soma piaZelensky alaani mauaji ya mateka kukatwa vichwa

Kufuatia video hiyo Jumuia mbalimbali za Kimataifa Ikiwemo Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu nchini Ukraine, Umoja wa Ulaya wameshtushwa na video hiyo wakisema ni mauaji ya "Kikatili." Msemaji wa  Kremlin Dmitry Peskov amesema wanatilia shaka juu ya video hiyo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW