Zelensky atoa wito wa msaada zaidi wa ulinzi wa anga
19 Januari 2025Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa mara nyengine tena amewatolea mwito washirika wake kuipa nchi yake mifumo zaidi ya ulinzi wa anga ya Patriot inayotengenezwa Marekani, kufuatia mashambulizi zaidi ya 1000 ya Urusi yaliyofanyika ndani ya wiki nzima.
Kupita mtandao wa Telegram Zelensky amesema Ukraine inahitaji usaidizi thabiti kutoka kwa washirika wake.
Soma pia: Uingereza yaahidi kuihakikishia Ukraine usalama
Aidha Zelensky amesema Urusi iliishambulia Ukraine kwa mabomu,droni 550 na takriban makombora 33 na kuchapisha video inayoonyesha uharibifu baada ya mashambulizi, katika mji wa Kiev, Zaporizhzhya na mkoa wa Donbass mashariki mwa Ukraine.
Ukraine imekuwa ikijilinda dhidi ya Urusi tangu uvamizi wa Februari 2022. Mwishoni mwa wiki wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema vikosi vyake vimepiga hatua zaidi upande wa Mashariki.
Soma pia: Zelensky asema "kutotabirika" kwa Trump kunaweza kumaliza vita