1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky autangaza 'mpango wa ushindi' Ulaya

11 Oktoba 2024

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amewatembelea washirika wake wa Ulaya kupigia upatu kile anachokiita "mpango wa ushindi" wa nchi yake dhidi ya Urusi kwenye vita vinavyoendelea kwa mwaka wa pili sasa.

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine.
Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine.Picha: Daniel Roland/AFP/Getty Images

Hapo jana aliwasili mjini Paris kukutana na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, akitokea Uingereza alikofanya mazungumzo na Waziri Mkuu Keir Starmer.

Kwenye mkutano wao na waandishi wa habari mjini Paris, Zelensky alikanusha vikali uvumi kwamba nchi yake inaweza kukubaliana na ushauri wa kusitisha mapigano.

Soma zaidi: Makombora ya Urusi yauwa 6 Odessa

Baadaye, Zelensky aliekelea Rome, ambako alikutana na kuzungumza na Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni.

Hivi leo, rais huyo wa Ukraine anatazamiwa kuwa na mkutano wa faragha na kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis, kwenye makao yake makuu, Vatican.