1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky awahimiza viongozi wa EU kuridhia uanachama wake

14 Desemba 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy leo amehimiza mkutano wa kilele wa viongozi wa Umoja wa Ulaya unaofanyika mjini Brussels kuanza mazungumzo ya uanachama wake katika Umoja huo.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: AFP/Getty Images

Akihutubia mkutano huo kwa njia ya video, Zelensky amewaomba viongozi hao kutowasaliti watu na imani yao kwa Ulaya.

Zelenskyameongeza kuwa leo ni siku muhimu na kwamba iwapo itakuwa njema ama mbaya kwa nchi hiyo, matukio yake yataingia katika historia.

Soma pia:Zelensky ahimiza nchi wanachama wa EU na Marekani kuipa Ukraine misaada zaidi ya kifedha

Miongoni mwa viongozi wa mataifa 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya, ni waziri mkuu wa Hungary pekee Viktor Orban aliyepinga kuanzishwa kwa mazungumzo hayo na Ukraine wakati taifa hilo linapoendelea kukabiliana na uvamizi wa Urusi.

Kwakuwa maamuzi kama hayo yanahitaji kuungwa mkono na mataifa yote wanachama, Umoja wa Ulaya hauwezi kuruhusu kujumuishwa kwa Ukraine  bila kuidhinishwa na  Orban.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW