1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Zelensky awasifu wanajeshi wake kwa kudungua ndege za Urusi

26 Desemba 2023

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amewasifu wanajeshi wa nchi yake kufuatia ripoti kwamba ndege za kivita za Urusi zimekuwa zikidunguliwa kwenye uwanja wa vita.

Ndege ya kivita ya Urusi, Sukhoi 30
Ndege ya kivita ya Urusi, Sukhoi 30 Picha: Alexander Strela/Zoonar/picture alliance

Inaarifiwa katika kipindi cha wiki moja iliyopita vikosi vya Ukraine vimefanikiwa kudungua ndege 5 za kivita za Urusi aina ya Sukhoi chapa Su-34 na Su-30.

Kupitia hotuba ya kila siku kwa taifa, Zelensky amesema taarifa hizo "ni mafanikio ya kutia moyo" na amewaonya marubani wa Urusi kwamba ulinzi wa anga ya Ukraine utaimarika zaidi siku za usoni pale taifa litakapopokea ndege za kivita chapa F-16.

Mataifa kadhaa ya magharibi yameahidi kuipitia Ukraine ndege hizo mamboleo katika kipindi cha miezi michache inayokuja. 

Katika hatua nyingine upande wa Urusi umetangaza kwamba jeshi lake limeukamata mji wa Marinka uliopo mashariki mwa Ukraine baada ya miezi kadhaa ya mapambano. Hata hivyo Ukraine imesema madai hayo ni ya uongo kwa sababu mapigano bado yanaendelea.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW