1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky awasili Japan kwa mazungumzo na viongozi wa G7

20 Mei 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amewasili nchini Japan leo kwa mazungumzo ya kidiplomasia na viongozi wa kundi la mataifa tajiri na ya kidemokrasia la G7 wanaokutana tangu jana kwenye mji wa Hirishoma.

Mkutano wa G7 HiroshimaJapan | Volodymyr Zelensky akutana na Giorgia Meloni
Baada ya kuwasili Hiroshima, Zelensky amefanya mkutano na waziri mkuu wa Italia, Giorgia Meloni. Picha: Ludovic Marin/POOL/AFP/Getty Images

Japan iliyo mwenyeji wa mkutano huo wa kilele, imesema uamuzi wa Zelensky wa kufika Hiroshima unatokana na "shauku kubwa" ya kushiriki mazungumzo na viongozi wa G7 na mataifa mengine yanayoweza kupigia upatu ulinzi wa Ukraine dhidi ya hujuma kutoka Urusi.

Kwenye mazungumzo hayo, Zelensky anatumai kuimarisha uungaji mkono wa kimataifa katika wakati Ukraine inajiandaa kwa operesheni ya kujibu mapigo ili kuyarejesha maeneo yote yaliyonyakuliwa na Urusi.

Ziara yake inafanyika saa chache baada ya kundi la G7 kutangaza nia ya kuongeza mbinyo dhidi ya Urusi kupitia vikwazo vya kiuchumi ili kuiadhibu dola hiyo kwa uvamizi wake wa zaidi ya mwaka mmoja nchini Ukraine.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW