1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky awasili Oslo kwa mkutano na mataifa ya Scandinavia

13 Desemba 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, amewasili mjini Oslo, Norway mapema leo kwa mazungumzo na viongozi wa nchi tano za ukanda wa Nordic.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.Picha: AFP/Getty Images

Nchini hizo ni Denmark, Finland, Iceland, Norway na Sweden, ambazo ni miongoni mwa wafadhili wake wakuu katika vita vyake dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Waziri Mkuu wa Norway Jonas Gahr Store, amemuhakikishia Zelensky kwamba nchi yake itaendelea kuunga mkono ulinzi wa Ukraine.

Hapo awali, Rais Zelensky alipokuwa akimaliza ziara yake nchini Marekani alisema nchi yake imefanikiwa katika kukabiliana na uvamizi wa Urusi, ingawa amesisitiza umuhimu wa umoja dhidi ya uchokozi wa Urusi.

Katika Ikulu ya Marekani, White House hapo jana, Zelensky alisema ziara yake ina lengo la kuyaelezea yaliyo muhimu, hasa jinsi ya kuishinda Urusi kwenye vita vya angani.

Hayo yakijiri, takriban watu 45 wameripotiwa kujeruhiwa usiku wa kuamkia leo baada ya Urusi kuushambulia mji wa Kiev kwa makombora.