1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPoland

Zelensky awasili Poland kwa ziara ya nadra nje ya Ukraine

5 Aprili 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amewasili leo katika nchi jirani Poland, ikiwa ni safari ya karibuni kabisa kati ya ziara zake za nadra za nje ya nchi tangu uvamizi wa Urusi nchini humo.

Poland, Warsaw | Ziara ya Rais Volodomyr Zelensky
Rais Volodomyr Zelensky (kushoto) na mkewe Olena wakikaribishwa na rais Andrzej Duda wa Poland na mkewe mjini Warsaw.Picha: Wojtek Radwanski/AFP/Getty Images

Poland, mwanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO ambayo inapakana na Ukraine ni mshirika muhimu wa ulinzi wa Kyiv dhidi ya Urusi na inawahifadhi Waukraine waliomiminika nchini humo wakikimbia vita.

Wakati wa ziara yake, Zelensky atakutana na mwenzake wa Poland, Andrzej Duda na pia kuhutubia katika eneo la kihistoria la katikati mwa mji mkuu wa Poland Warsaw.

Pia mazungumzo na Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki yamepangwa. Tangu kuanza kwa uvamizi kamili wa Urusi Februari 2022, Zelensky amezuru Washington, London, Paris na Brussels.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW