1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky: Bado ninayo nia ya kufanya uchaguzi Ukraine

Hawa Bihoga
29 Agosti 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema bado ana nia ya kufanya uchaguzi mkuu licha ya uvamizi wa Urusi nchini humo, lakini ameonya kwamba msaada wa kifedha unahitajika kutoka Marekani na Umoja wa Ulaya.

Ukraine Präsident Selentskji
Picha: Ukrainian Presidency/abaca/picture alliance

Kwa mujibu wa sheria za Ukraine ni marufuku kufanya uchaguzi chini ya sheria za kijeshi na kwa hatua hiyo, taifa hilo ambalo bado lipo katika mapigano ya zaidi ya mwaka mmoja na jirani yake Urusi, linapata ugumu kuingia katika mchakato wa kideomocrasia litalazimika kuomba msaada wa kifedha kutoka kwa washirika wake Marekani na Umoja wa Ulaya kuendesha mchakato huo.

Katika mahojiano yaliorushwa siku ya Jumapili Zelensky amesema, licha ya nia yake ya uchaguzi  hawezi kuendesha zoezi hilo kwa njia ya mkopo, wala hatatoa fedha kwenye bajeti ya  ulinzi kwa ajili ya uchaguzi na badala yake bunge litapaswa kubadili "haraka iwezekeanvyo" sheria zinazotumika.

Soma pia:Zelensky ahimiza washirika wake kuharakisha mpango wa kuipa nchi yake ndege za kivita F-16

Alisema wanajeshi wapo mstari wa mbele kupigania democrasia, na kuwanyima fursa hiyo kwa sababu ya vita hiyo sio haki.

"Hii ndio sababu ilinifanya kupinga uchaguzi." Alisema

Ameongeza kwamba "ikiwa bunge linaelewa kwamba tunahitaji kufanya uchaguzi basi libadilishe sheria haraka"

Alisisitiza kwamba kitu cha muhimu hasa ni "kujitosa kwa pamoja, waangalizi lazima wafike katika maeneo tete."

Zelensky ameongeza kwamba, itakuwa ni muhimu kuhakikisha mamilioni ya wakimbizi wa Ukraine waliokimbilia kote katika mataifa ya Ulaya watashiriki katika zoezi hilo.

Zelensky: Bado ipo suluhu ya kisiasa Crimea

Akizungumzia mzozo baina ya Ukraine na Urusi hasa katika rasi ya Crimea ambayo ilitwaliwa na Moscow tangu mwaka 2014, alisema majadiliano ya kisiasa yatayolenga kupata suluhu yanawezekana kwani itahusisha waathiriwa wachache.

Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: ROB ENGELAAR/AFP

Alisema hataki kuhamishia vita katika ardhi ya Urusi, kwani lengo lake ni kukomboa maeneo ya Ukraine.

akizungumzia maendeleo kwenye uwanja wa mapambano alisema kusonga mbele hadi nchini Urusi kungelihatarisha kupoteza misaada muhimu kutoka kwa washirika wake wa Magharibi.

Soma pia:Zelensky asema upo uwezekano wa makubaliano juu ya Crimea

Mataifa ya Magharibi yameipatia Ukraine mabilioni ya dola ikiwa ni msaada wa kijeshi na fedha taslimu, tangu Urusi ilipoivamia kijeshi mnamo Febriari 2022.

Hata hivyo waenezaji propaganda wa urusina waungaji mkono wa vita hivyo wameonya mara kwa mara kwamba, iwapo itashindwa katika vita hivyo, Urusi inaweza kugawanywa na kukaliwa kwa mabavu na majeshi ya kigeni.

Urusi: Tumezima shambulio la Kiev

Wizara ya Ulinzi Urusi imesema jeshi limezima shambulio jingine la serikali ya Kiev kutekeleza kile ilichokiita shambulio la kigaidikwa kombora ambalo liliharibiwa huko kwenye Bahari Nyeusi karibu na pwani ya Crimea.

Hivi karibuni Ukraine imeongeza mashambulizi yake Crimea, huku ilipeleka kikosi cha makomando kwenye rasi hiyo wiki iliopita.

Viongozi wa Afrika wataka kumaliza mzozo wa Ukraine

02:31

This browser does not support the video element.

Wachambuzi wanasema hatua hiyo ya Kiev ni katika jaribio la kuharibu njia za usambazaji za vikosi vya Moscow vinavyokalia kimabavu eneo la kusini mwa Ukraine na kushambulia maghala ya silaha na mafuta.

Soma pia:Urusi yasema imedungua droni mbili za Ukraine mjini Moscow

Naibui waziri wa Ulinzi Ukraine Hanna Maliar amesema , Urusi bado inadhibiti zaidi ya kilomita za mraba laki moja nchini Ukraine ikiwa ni pamoja na eneo la Crimea.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW