1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Zelensky: Hakuna maana yoyote kufanya mazungumzo na Putin

28 Agosti 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema mazungumzo ya amani na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin hayatakuwa na "maana yoyote."

Wolodymyr Zelensky in Spanien bei Pedro Sánchez
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Juan Carlos Rojas/picture alliance

Akizungumza katika hafla iliyofanyika mjini Kyiv, Zelensky amesema dunia inaisubiri Ukraine kuwasilisha mpango wa maafikiano kuhusu jinsi ya kuvimaliza vita kati yake na Urusi.

Kiongozi huyo ameeleza kwamba, hakuna maana yoyote ya kufanya mazungumzo na Putin kwa sababu rais huyo wa Urusi hataki kuvimaliza vita hivyo kwa njia ya kidiplomasia.

Soma pia: Ukraine yasema haina nia ya kulikalia eneo la Kursk huko Urusi

Zelensky hata hivyo amesema Putin anaweza tu kuwa tayari kushiriki mazungumzo japo kwa sharti la Ukraine kutambua hatua ya Moscow kuikamata asilimia 30 ya ardhi ya Ukraine.

Amesema vikosi vyake kuingia katika jimbo la kusini mwa Urusi la Kursk kumewanyamazisha wakosoaji wake na kwamba ni "sehemu ya mpango wa ushindi" ambao atauwasilisha kwa Rais wa Marekani Joe Biden mwezi ujao.