1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky: Kipindi cha baridi Ulaya kitakuwa kigumu

Zainab Aziz Mhariri: Amina Abubakar
4 Septemba 2022

Rais wa Ukraine Volodmyr Zelensky amezitahadharisha nchi za magharibi kwamba kipindi cha baradi kijacho barani Ulaya kinaweza kuwa kigumu kutokana na Urusi kuchukua hatua za kukata ugavi wa gesi na mafuta kwa nchi hizo.

Ukraine Kiew | Wolodymyr Selenskyj, Präsident
Picha: Ukrainian Presidential Press Off/Planet Pix via Zuma/picture alliance

Kwa mara nyingine kinu cha nyukulia cha Zapozhizhya kimekuwa uwanja wa mapambano kusini mwa Ukraine licha ya uwepo wa ujumbe wa shirika la kudhibiti matumizi ya nishati ya nyukilia IAEA. Shirika hilo limesema ugavi wa umeme ulikatwa. Voymbo vya habari vya Urusi viliripoti hapo awali kwamba njia za umeme ziliharibiwa kutokana na mapigano na kwamba ugavi wa umeme kwa ajili ya maeneo  yanayodhitiwa na Ukraine ulikatizwa.

Ujumbe wa shirika la kudhibiti matumizi ya nishati ya nyukilia IAEA ulipozuru kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia nchini Ukraine.Picha: D. Candano Laris/IAEA/dpa/picture alliance

Hata hivyo Urusi imezungumzia juu ya vikwazo vilivyowekwa dhidi yake na nchi za maghgaribi kuwa ndio vilivyosababisha matatizo ya kiufundi na kutifua mvurugiko katika ugavi wa nishati.

Nchi za Ulaya zinazoiunga mkono Ukraine kijeshi na kidiploma zimeilaumu Urusi kwa kutumia nishati kama silaha ya kivita. Baadhi ya wachamabuzi wamesema kupanda kwa gharama za maisha wakati msimu wa baridi unakaribia kunaweza kudhoofisha msaada unaotolewa na nchi za magharibi kwa ajili ya serikali ya Ukraine.

Soma zaidi:IAEA kuweka ujumbe wa kudumu katika kinu cha Zaporizhzhia

Serikali za nchi za magharibi huenda zikalemewa na malalamiko ya wananchi wao. Wiki iliyopita Urusi ilisema italifunga bomba la kwanza la gesi lililoleta nishati hiyo nchini Ujerumani.

Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Frederic Kern/Future Image/IMAGO

Nchi saba tajiri duniani za kundi la G7 zilitangaza kuweka kikomo katika bei ya mafuta kutoka Urusi. Urusi imesema haitauza mafuta kwa nchi yoyote inayotekeleza agizo hilo la nchi hizo saba tajiri. Kutokana na hali hiyo Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema Urusi si mshirika wa kuaminika tena.

Vyanzo: RTRE/DPA

 

 

 

 

 

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW