1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky kuhutubia mkutano wa G7

6 Desemba 2023

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine atajiunga leo kwenye mkutano wa kilele kwa njia ya video na viongozi wa kundi la G7 linaloundwa na nchi saba tajiri duniani.

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine atashiriki mkutano wa G7 kwa njia ya video.
Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine atashiriki mkutano wa G7 kwa njia ya video.Picha: AFP/Getty Images

Zelensky atahudhuria sehemu ya kwanza ya mkutano huo utakaoongozwa na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida.

Ikiwa karibu miaka miwili baada ya uvamizi wa Urusi, dalili zinaongezeka kuwa uungaji mkono wa Ukraine kutoka kwa Magharibi unapungua wakati ambapo mapambano ya jeshi la Urusi yakionekana kuyumba, na wakati mapato ya mafuta ya Rais Vladmir Putin yakiimarika.

Soma zaidi: Zelensky kuwahutubia maseneta wa Marekani kufuatia msaada uliozuiliwa

Zelensky jana alifanya uamuzi wa ghafla wa kutohudhuria mkutano mwengine wa vidio hapo jana na maseneta wa Marekani.

Bunge la Marekani limegawanyika zaidi kuhusu uungaji mkono wa Ukraine kuliko ilivyokuwa wakati mwingine wowote katika vita hivyo, huku nchi hiyo ikionekana kuumaliza haraka msaada wa kujeshi uliotolewa na Marekani mpaka sasa. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW