1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky kwenda Uswisi kuimarisha uungaji mkono wa kimataifa

15 Januari 2024

Rais Volodymyr Zelensky anakwenda nchini Uswisi leo akiwa na dhamira ya kuendelea kuimarisha uungaji mkono zaidi kutoka kwa washirika wake katika wakati vita baina ya Ukraine na Urusi vinakaribia mwaka wa pili.

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine
Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine.Picha: AFP/Getty Images

Tangazo la ziara hiyo limetolewa na ofisi ya kiongozi huyo usiku wa kuamkia leo.

Akiwa nchini Uswisi Zelensky atakutana na viongozi wakuu wa mabaraza mawili ya bunge la nchi hiyo, viongozi wa vyama vya siasa pamoja na rais wa Uswisi na kisha kuhudhuruia Kongamano la Uchumi duniani linalofunguliwa leo huko kwenye mji wa Davos.

Ziara hiyo ilitangazwa saa chache baada ya Ufaransa na Ujerumani kusisitiza azma yao ya kuendelea kuiunga mkono Ukraina katika vita dhidi ya Urusi.

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi hizo mbili, wamesema kwa nyakati tofauti kuwa watakuwa pamoja na Ukraine kwa muda mrefu kadri itakavyohitajika.