1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky kukutana na Meloni mjini Roma

Josephat Charo
15 Aprili 2026

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amewasili mjini Roma nchini Italia Jumatano kwa mazungumzo huku akiwashinikiza washirika wa Ulaya kuongeza ulinzi wa anga wa nchi yake dhidi ya mashambulizi ya Urusi.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kukutana na Meloni mjini Roma
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kukutana na Meloni mjini RomaPicha: Koen van Weel/ANP/IMAGO

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky atakutana na Waziri Mkuu wa Italia Georgia Meloni, siku moja baada ya kuizuru Ujerumani, ambapo yeye na Kansela Ujerumani Friedrich Merz walikubaliana kuimarisha ushirikiano wa ulinzi, hasa katika vita vya ndege zisizo na rubani.

Zelensky amesema kipaumbele kikuu cha kidiplomasia cha Ukraine ni kupata msaada wa washirika wake kununua na kujenga mifumo zaidi ya ulinzi wa anga.

Ameyasema hayo Jumatano alipofanya mikutano na viongozi wa Ulaya, huku Urusi ikiendelea na mashambulizi yake mabaya dhidi ya raia na miundombinu ya umma nchini Ukraine.

Zelenskyy alikuwa akitembelea miji mitatu mikuu ya Ulaya katika saa 48, akihakikisha ahadi za msaada zaidi wa kijeshi na kifedha kutoka Ujerumani na Norway kabla ya safari yake kwenda Italia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW