1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Zelensky kukutana na Sanchez kwa mazungumzo mjini Madrid

16 Machi 2026

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, atafanya ziara fupi mjini Madrid siku ya Jumatano kwa mazungumzo na Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez.

Spanien Madrid | Pedro Sanchez na Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiwa na Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez. Picha: Oscar del Pozo/AFP

Duru kutoka ofisi ya Waziri Mkuu huyo zimesema Zelensky, atasaini makubaliano kadhaa na kuwa na mkutano wa pamoja na waandishi habari na Sanchez, katika ziara yake hiyo ambayo ni ya nne  nchini humo tangu Urusi ilipoivamia Kiev mwaka 2022.

Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi zake za kupata uungwaji mkono wa kidiplomasia na kijeshi kutoka kwa washirika wa Ukraine wa Magharibi katika vita hivyo vilivyoingia mwaka wake wa tano.

Mwezi Novemba, Zelensky alipata msaada mpya wa kijeshi uliogharimu dola milioni 706 kutoka Uhispania baada ya kukutana na Waziri Mkuu Pedro Sanchez mjini Madrid.

Marekani imekuwa ikiendelea kuishinikiza Kyiv na Moscow kuingia katika makubaliano ya amani lakini mazungumzo ya pande tatu ya kujaribu kufikia hilo yamekwama kufuatia vita vya Mashariki ya Kati.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW