SiasaUkraine
Zelensky kukutana na Trump Ijumaa kujadili masuala ya silaha
16 Oktoba 2025
Matangazo
Vyanzo mbalimbali vimeeleza kuwa mazungumzo ya Trump na Zelenskyyatajikita katika suala la kuipatia Kiev makombora ya masafa marefu ya Tomahawks na yale ya Patriots.
Hayo yakiarifiwa, Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz amesema ataushinikiza Umoja wa Ulaya kutumia mali za Urusi zilizozuiwa ili kuipatia Ukraine mkopo:
" Tunataka kuzitumia vyema mali zilizozuiwa za benki kuu ya Urusi kwa kuipa Ukraine jumla ya euro bilioni 140 kama mkopo wa ziada usiyo na riba."
Aidha, Ujerumani pia imeahidi kuipatia Ukraine msaada zaidi wa kijeshi wenye thamani ya dola bilioni 2 mwaka ujao ili kuiwezesha kuendelea kuikabili Urusi.